Wednesday, November 29, 2017

DUA KWENYE QUR-AN NA TAFSIRI YAKE


 رَبِّ اجْعَلْ هَـَذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُق ْأَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُم بِاللّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ     (البقرة:126)
Ee Mola wangu! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho. (Al-Baqarah: 126)
رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ      
رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَآ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ (البقرة 127- 128)
Ewe Mola wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi.
Ewe Mola wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongonI'm i mwa vizazi vyetu wawe ummah uliosilimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. (Al-Baqarah: 127-128)).

رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ (البقرة 201  )  
Mola wetu, tupe duniani mema, na Aakhirah mema, na utulinde na adhabu ya Moto. (Al-Baqara 201)

رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ (البقرة 250 )
Mola wetu! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie tuwashinde watu Makafiri (Al-Baqarah: 250)

رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلاَ تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلاَ تُحَمِّلْنَا مَا لاَ طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنتَ مَوْلاَنَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ  (البقرة 286)
Mola wetu! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Usitutwike tusiyoyaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri. (Al-Baqarah: 286)

رَبَّنَا لاَ تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ  (آل عمران 8  )
Mola wetu! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwishatuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mpaji. (Al-'Imraan: 8)

رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ  (آل عمران 16)
Mola wetu! Hakika sisi tumeamini, basi tufutie madhambi yetu, na tuepushe na adhabu ya Moto.  (Al-Imran 16)

رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنْكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاء  (آل عمران 38]
Mola wangu! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unayesikia maombi. (Al-'Imraan: 38) 

رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنزَلَتْ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ  (آل عمران 53)
Mola wetu! Tumeyaamini uliyoyateremsha, na tumemfuata huyu Mtume, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (Al-'Imraan: 53)

ربَّنَا اغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِي أَمْرِنَا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَِ    (آل عمران 147)    
Mola wetu! Tughufirie madhambi yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru tuwashinde kaumu ya makafiri (Al-'Imraan: 147)

رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَذا بَاطِلاً سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلإِيمَانِ أَنْ آمِنُواْ بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الأبْرَارِ رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَى رُسُلِكَ وَلاَ تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّكَ لاَ تُخْلِفُ الْمِيعَاد ِ
(آل عمران 191-194)
Mola wetu! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto. 
Mola wetu! Hakika unaye mtia Motoni umemhizi; na waliodhulumu hawana wasaidizi.
Mola wetu! Hakika sisi tumemsikia mwenye kuita akiitia Imani kwamba: Muaminini Mola wenu; nasi tukaamini. Basi tusamehe madhambi yetu, na utufutie makosa yetu, na utufishe pamoja na watu wema.
Mola wetu! Na utupe uliyotuahidi kwa Mitume wako, wala usituhizi Siku ya Qiyaamah. Hakika Wewe huvunji miadi. (Al-'Imraan :191-194) 

 رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا  (النساء:75)
Mola wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anayetoka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako. (An-Nisaa: 75)
رَبَّنَا آمَنَّا فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ   (المائدة:83)
Mola wetu! Tumeamini. Basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (Al-Maaidah:  83)

رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ    (الأعراف23) 
Mola wetu! tumejidhulumu nafsi zetu, na kamahutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika  (Al-A'raaf: 23)

رَبَّنَا لاَ تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (الأعراف 47)   
Mola wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na watu waliodhulumu (Al-A'raaf: 47)

رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ خَيْرُ الْفَاتِحِينَ   (الأعراف:89)
Ewe Mola wetu! Tuhukumie baina yetu na kaumu yetu kwa haki, nawe ndiye mbora wa wanaohukumu.  (Al-A'raaf: 89) 

رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ  ( الأعراف 126)
Ewe Mola wetu! Tumiminie uvumilivu na utufishe hali ni Waislamu. (Al-A'raaf: 126)

أَنتَ وَلِيُّنَا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الْغَافِرِينَ (الأعراف 155)         
Wewe ndiye Rafiki Mlinzi wetu. Basi tughufirie na uturehemu. Na Wewe ndiye mbora wa kughufiria (Al-A'raaf: 155)

حَسْبِيَ اللّهُ لا إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ (التوبة  129) 
Allaah ananitosheleza. Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye tu. Mimi namtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola wa 'Arsh tukufu. (At-Tawbah: 129)

رَبَّنَا لاَ تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ   (يونس85-86)
Ewe Mola wetu! Usitufanye wenye kutiwa misukosuko na hao watu madhaalimu. 
Na utuokoe kwa rehema yako na watu makafiri  (Yuwnus: 85 – 86 )

رَبِّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَسْأَلَكَ مَا لَيْسَ لِي بِهِ عِلْمٌ وَإِلاَّ تَغْفِرْ لِي وَتَرْحَمْنِي أَكُن مِّنَ الْخَاسِرِينَ   (هود  74)
Ewe Mola wangu! Mimi najikinga kwako nisikuombe nisio na ujuzi nalo. Na kamahunisamehe na ukanirehemu, nitakuwa katika waliopata khasara. (Huwd: 47)

رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلاَةِ وَمِن ذُرِّيَّتِي رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَاء    (إبرهيم-40)
Mola wangu! Nijaalie niwe mwenye kusimamisha Swalaah, na katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu, na ipokee dua yangu. (Ibraahiym: 40)

رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَاب   (إبرهيم41 )  
Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu(Ibraahiym: 41)

أَنتَ وَلِيِّي فِي الدُّنُيَا وَالآخِرَةِ تَوَفَّنِي مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ  (يوسف:101)
Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Aakhirah. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na nichanganyishe na watendao mema(Yuwsuf: 101)

رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِيصَغِيرًا (الإسراء 24)
Mola wangu! Warehemu kama walivyo nilea utotoni. (Al-Israa: 24)

 رَّبِّ أَدْخِلْنِي مُدْخَلَ صِدْقٍ وَأَخْرِجْنِي مُخْرَجَ صِدْقٍ وَاجْعَل لِّي مِن لَّدُنكَ سُلْطَانًا نَّصِيرًا   (الإسراء-80)   
Mola wangu! Niingize muingizo mwema, na unitoe kutoka kwema. Na unipe nguvu zinazo toka kwako zinisaidie. (Al-Israa: 80)

رَبَّنَا آتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا (الكهف10) 
Mola wetu! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uongofu katika jambo letu. (Al-Kahf: 10) 

رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي  وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي  وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِّن لِّسَانِي يَفْقَهُوا قَوْلِي (طه 25-28)  
Ewe Mola wangu! Nikunjulie kifua changu,
Na unifanyie nyepesi kazi yangu,
Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu.(Twaahaa: 25-28)

 رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا (طه 114)  
Mola wangu! Nizidishie ilimu. (Twaahaa: 114)

لا إِلَهَ إِلا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ (الأنبياء87) 
Hapana mabudiwa wa haki isipokuwa Wewe Subhaanaka Uliyetakasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. (Al-Anbiyaa: 87)

رَبِّ لاَ تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ   (الأنبياء 89 )  
Mola wangu! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanaorithi 
(Al-Anbiyaa: 89)

رَبِّ أَنْزِلْنِي مُنْزَلاً مُبَارَكاً وَأَنْتَخَيْرُ الْمُنْزِلِينَ (المؤمنون 29)
Mola wangu! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora wa wateremshaji (Al-Mu'minuwn 29)

رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ (المؤمنون97-98) 
Mola wangu! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani.  Na najikinga kwako, Mola wangu, wasinikaribie. (Muuminuwn: 97-98)

  رَبَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ (المؤمنون  109)  
Mola wetu! Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanaorehemu. (Muuminuwn: 109)

رَّبِّ اغْفِرْ وَارْحَمْ وَأَنتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ (المؤمنون 118)
Mola wangu! Samehe na urehemu nawe ni Mbora wa wanaorehemu 
(Al-Muuminuwn: 118)

رَبِّ هَبْ لِي حُكْماً وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ   وَاجْعَلْ لِي لِسَانَ صِدْقٍ فِي الأَخِرِين 
 وَاجْعَلْنِي مِنْ وَرَثَةِ جَنَّةِ النَّعِيمِ  (الشعراء 83-85)
Mola wangu! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema. Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadayeNa unijaalie katika warithi wa Bustani za neema. (Ash-Shu'araa: 83-85)
رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْلِي (القصص 16)
Mola wangu! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu; basi nisamehe (Al-Qaswas: 16)

رَبِّ بِمَا أَنْعَمْتَ عَلَيَّ فَلَنْ أَكُونَظَهِيرًا لِلْمُجْرِمِينَ (القصص 17)
Mola wangu! Kwa ulivyonineemesha, basi mimi sitokuwa kabisa msaidizi wa wakosefu (Al-Qaswas: 17)
رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ(القصص 21)
Mola wangu! Niokoe na watu madhaalimu(Al-Qaswas: 21)

رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَاماً الفرقان 65 )
Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi (Al-Furqan 65)

  رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَاماً (الفرقان 74)
Mola wetu! Tupe katika wake zetu na wetoto wetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachaji Allaah. (Al-Furqaan: 74)

رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَى وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحاً تَرْضَاهُوَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ (النمل 19)
Ee Mola wangu! Nizindue niishukuru neema yako uliyonineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema. (An-Naml: 19) 
وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللَّهِ إِنَّ اللَّهَبَصِيرٌ بِالْعِبَادِ  (غافر 44
Nami namkabidhi Allaah mambo yangu. Hakika Allaah Anawaona waja wake.(Ghaafir: 44)

رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَالَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَى وَالِدَيَّوَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُوَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي إِنِّيتُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنْ الْمُسْلِمِينَ  (الأحقاف 15)
Mola wangu! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu. (Al-Ahqaaf: 15)

رَبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ  (الدخان 12)  
Mola wetu! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. (Ad-Dukhaan: 12)

 رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالإِيمَانِ وَلاَ تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَؤُوفٌ رَّحِيمٌ  (الحشر 10)
Mola wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola wetu! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu. (Al-Hashr: 10)
 رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَاوَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ  
 رَبَّنَا لاَ تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلَّذِينَكَفَرُوا وَاغْفِرْ لَنَا رَبَّنَا إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (الممتحنة 4-5)
Mola wetu! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo.
Mola wetu! Usitufanyie mtihani kwa waliokufuru. Na tusamehe, Mola wetu. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima(Al-Mumtahina: 4 -5 )
 رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (التحريم 8)  
Mola wetu! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu .(At-Tahriym: 8)
 رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا تَبَارًانوح:28)
Mola wangu! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliyeingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea. (Nuwh: 28)

TAWHIYD


Mfano Wa Neno Zuri (La Tawhiyd) Ni Kama Mti Mzuri (Mtende) Na Faida Zake 
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

 ((أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللّهُ مَثَلاً كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاء))  
 ((تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا وَيَضْرِبُ اللّهُ الأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ))
((Hebu hukuona vipi Allaah Alivyopiga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni)) 

((Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake. Na Allaah Huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka)) [Ibraahiym: 24 25]  

((وَمَثلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِن فَوْقِ الأَرْضِ مَا لَهَا مِن قَرَار))  
(( يُثَبِّتُ اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ وَيُضِلُّ اللّهُ الظَّالِمِينَ وَيَفْعَلُ اللّهُ مَا يَشَاء))  
((Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, uliong'olewa juu ya ardhi. Hauna imara))   

((Allaah Huwatia imara wenye kuamini kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotea hao wenye kudhulumu. Na Allaah Hufanya Apendavyo)) [Ibraahiym:  26-27] 

Aayah hizi tukufu zina mafunzo muhimu kwetu yanayohusu Tawhiyd, (Kumpwekesha Allaah bila kumshirikisha na chochote) kuthibitika kauli duniani na Aakhirah na pia kutuonyesha tofauti ya matunda yanayotokana baina ya  maneno mawili haya; neno la tawhiyd kuwa matunda yake ni kheri tupu, na neno la kufru kuwa matunda yake ni mabaya hayana thamani wala faida yoyote bali ni shari tupu. 

'Aliy bin Abiy Twalhah amesimulia kwamba 'Abdullaah bin 'Abbaas amesema kuhusu: 

((كَلِمَةً طَيِّبَة)) 
 ((neno zuri))

ina maana ni kushuhudia: 'Laa ilaaha illa-Allaah' (Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah). 

((كَشَجَرةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاء))    ((تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا))
((Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni)) 
((Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake))

'Abdullaah bin 'Abbaas amesema kuhusu ((Kama mti mzuri)) "ni mti wa Peponi" [At-Twabariy 16:573]

Ad-Dhwahaak, Sa'iyd bin Jubayr, 'Ikirimah, Mujaahid na wengineo wamesema, maana ya mfano huu wa huo mti mzuri unaotoa matunda yake kila mara, ni kama Muumini ambaye naye hufanya vitendo vyema kila mara usiku na mchana navyo vinapanda juu kila mara mchana na usiku. [At-Twabariy 16:572-573]

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametutajia huo mti khaswa jina lake kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo:

عَنْ اِبْن عُمَر قَالَ : كُنَّا عِنْد رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ   ((أَخْبِرُونِي عَنْ شَجَرَة تُشْبِه - أَوْ - كَالرَّجُلِ الْمُسْلِم لَا يَتَحَاتّ وَرَقهَا صَيْفًا وَلَا شِتَاء وَتُؤْتِي أُكُلَهَا كُلّ حِين بِإِذْنِ رَبّهَا ))  قَالَ اِبْن عُمَر : فَوَقَعَ فِي نَفْسِي أَنَّهَا النَّخْلَة وَرَأَيْت أَبَا بَكْر وَعُمَر لَا يَتَكَلَّمَانِ فَكَرِهْت أَنْ أَتَكَلَّمَ فَلَمَّا لَمْ يَقُولُوا شَيْئًا قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ   ((هِيَ النَّخْلَة))   فَلَمَّا قُمْنَا قُلْت لِعُمَرَ : يَا أَبَتَاهُ وَاَللَّه لَقَدْ كَانَ وَقَعَ فِي نَفْسِي أَنَّهَا النَّخْلَة قَالَ مَا مَنَعَك أَنْ تَتَكَلَّم ؟ قُلْت لَمْ أَرَكُمْ تَتَكَلَّمُونَ فَكَرِهْت أَنْ أَتَكَلَّم أَوْ أَقُول شَيْئًا قَالَ عُمَر : لَأَنْ تَكُون قُلْتهَا أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ كَذَا وَكَذَا  -  البخاري
Kutoka kwa ibn 'Umar ambaye amesema: "Tulikuwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: ((Niambieni kuhusu mti unaofanana au kama Muislamu, ambao majani yake hayaanguki wakati wa majira ya joto wala wakati wa majira ya baridi na hutoa matunda yake kila mara kwa idhini ya Mola wake)) Ibn 'Umar akasema: "Niliufikiria kuwa ni mtende, lakini niliona haya kujibu nilipoona  Abu Bakar na 'Umar hawakujibu. Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ni mtende)). Tulipoondoka, nilimwambia 'Umar: Ewe baba yangu, WaLLaahi nilidhani kuwa ni mtende". Akasema: "Kwa nini basi hukutaja?" Nikasema: "Nilikuoneni kimya nikachukia (nikaona vibaya) kusema kitu". Akasema 'Umar: "Ungelisema ingelikuwa bora kwangu kuliko kadhaa na kadhaa" (Yaani ningelikuwa na fakhari zaidi kuwa wewe mwanangu ndiye uliyeweza kujibu pekee.  [Al-Bukhaariy] 

 Hebu basi tutazame sifa za mti huu mzuri (mtende) na sifa za Muumimi tuone jinsi zilivyofanana: 

Mtende:
Umethibiti ardhini kwa mizizi yake
Muumini:
Anathibiti Iymaan yake daima na huwa na Iymaan ya hali ya juu.


Mtende:
Tunda lake ni zuri na tamu.
Muumini:
Mazungumzo na vitendo vyake ni vizuri na vya kupendeza, na si mwenye maneno maovu yanayoudhi, kudharau, kukashifu, kusengenya, kufitinisha n.k.

Mtende:
Umepambika vizuri na kufunikika. 
Muumini:
Mavazi yake ni mazuri ya heshima.

Mtende:
Ni wepesi kula tunda lake.
Muumini:
Ni wepesi kujadiliana na watu kwa hoja, dalili na kwa busara.

Mtende:
Una faida kwa anayekula, kwani matunda yake yana siha mwilini na huwa ni  kinga ya maradhi, uchawi, na kila aina ya maovu kwa kula tende saba asubuhi kama kula chochote   [Hadiyth kuhusu kula tende saba asubuhi katika Al-Bukhaariy na Muslim]   
Muumini:
Iimu yake anayotoa ina faida kubwa ya kuwaongoza Waislamu na wasio Waislamu kutoka upotofu kuingia katika uongofu na hivyo ni kuutakasa moyo  katika usalama wa shirki na maovu mengineyo, kinyume na moyo wenye maradhi ya shirki, unafiki n.k.
  
Mtende:
Ni mti madhubuti sana wenye kustahmili upepo mkali.
Muumini:
Iymaan yake imethibiti vizuri hata anapopata misukosuko na mitihani, huwa na moyo mkubwa wa kustahmili.

Mtende:
Kila unapokuwa mkubwa unazidi kutoa matunda na faida nyinginezo.
Muumini:
Kila anapozidi umri huongezeka elimu, busara na huzidi kunufaisha watu kwa kheri zake.

 Na Allaah Anajua zaidi



  


Huo ndio mfano wa neno zuri na mti mzuri. Ama mfano wa neno ovu na mti muovu kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) 

((وَمَثلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِن فَوْقِ الأَرْضِ مَا لَهَا مِن قَرَار))
 ((Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, uliong'olewa juu ya ardhi. Hauna imara.))  

Unaelezea kutokuamini kwa kafiri kuwa ni kama  mti usiokuwa madhubuti, mti mchungu kabisa, na bila shaka vitendo vyake havipandi juu wala havitakabaliwi. 


Kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema kuwa Humthibitisha mwenye kuamini katika maisha ya dunia na pia maisha ya Aakhirah kwa neno hilo lililothibiti kama mti, yaani 'Laa ilaaha illa-Allaah'.

((يُثَبِّتُ اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ وَيُضِلُّ اللّهُ الظَّالِمِينَ وَيَفْعَلُ اللّهُ مَا يَشَاء))
((Allaah Huwatia imara wenye kuamini kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotea hao wenye kudhulumu. Na Allaah Hufanya Apendavyo))


Duniani huthibiti kumuamini Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), kwa kuendesha maisha yake yote yakiwa katika mipaka ya Mola wake Mtukufu. Na nje ya maisha ya dunia huthibitika kwa kuweza kujibu maswali atakayoulizwa na Malaika wawili kaburini ambao ni Munkar na Nakiyr:     

عَنْ الْبَرَاء بْن عَازِب رَضِيَ اللَّه عَنْهُ أَنَّ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ  ((الْمُسْلِم إِذَا سُئِلَ فِي الْقَبْر شَهِدَ أَنْ لَا إِلَه إِلَّا اللَّه وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُول اللَّه فَذَلِكَ قَوْله (يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ"))) البخاري  وَرَوَاهُ مُسْلِم أَيْضًا وَبَقِيَّة الْجَمَاعَة
Imetoka kwa Al-Baraa bin 'Aazib (Radhiya-Llaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muislamu akiulizwa katika kaburi, atashuhudia kwamba: "Laa ilaaha Illa-Allaah wa Anna Muhammadar-Rasuulu-LLaah" (Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mjumbe wa Allaah) hivyo ndiyo maana ya kauli ya Allaah(Allaah Huwatia imara wenye kuamini kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika Aakhirah)) [Al-Bukhaariy, na katika usimulizi mwingine kutoka kwa Muslim na wengineo] 

Hadiyth nyingine imeelezea:  

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة قَالَ : قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ" ((يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاة الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَة))  قَال"(( ذَلِكَ إِذَا قِيلَ لَهُ فِي الْقَبْر مَنْ رَبّك وَمَا دِينك وَمَنْ نَبِيّك ؟ فَيَقُول رَبِّي اللَّه وَدِينِيّ الْإِسْلَام وَنَبِيِّي مُحَمَّد جَاءَنَا بِالْبَيِّنَاتِ مِنْ عِنْد اللَّه فَآمَنْت بِهِ وَصَدَّقْت فَيُقَال لَهُ صَدَقْت عَلَى هَذَا عِشْت وَعَلَيْهِ مُتّ وَعَلَيْهِ تُبْعَث))   
Kutoka  kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Allaah Huwatia imara wenye kuamini kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika Aakhirah).Akasema: ((Hivyo atakapoulizwa kaburini; Nani Mola wako, nini dini yako, nani Mtume wako? Atasema: Mola wangu ni Allaah, Dini yangu ni Islaam na Mtume wangu ni Muhammad, ametuletea dalili za wazi kutoka kwa Allaah, nikamuamini na nikamsadikisha. Ataambiwa: Umesema ukweli, umeishi kwa hayo, umefia kwa hayo na utafufuliwa kwa hayo)) [At-Twabariy: 16:596]

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atuthibitishe bil-qawlith-thaabit fil hayaatid-duniya wal-Aakhirah. (Atuthibitishe na kauli thabiti duniani na Aakhirah), Atujaalie tuwe Waumini wa kweli tuweze kufanya vitendo vyema daima vyenye kukubaliwa na Atuwezeshe kujibu maswali tutakayoulizwa kaburini.

SHEIKH SHARIF YUSSUF

HASAD KATIKA NDOA 1

HASAD KATIKA NDOA:  Baadhi ya watu hufanya chuki ama husda katika ndoa za watu kwa kutumia vitu mbalimbali, ikiwa kwa kusambaza maneno ya k...